MAHACKER WAIOBOMOA WEBSITE YA PROFESA JAY.....TEMBELEA UJIONEE
Watu wanaosadikika kuwa ni wahuni wa
kitechnolojia wameonekana kutenda mambo yao katika Official website ya
Daddy wa muziki wa rap Tanzania, Proffesa Jay http://www.professorjaytz.com/
ambayo kwa mujibu wake mwenyewe, site hii ilikuwa bado ipo katika
matengenezo na kuna mtu maalum ambaye alikuwa amemuasign kazi ya
kuitengeneza.
Hivi ndivyo site ya msanii huyu inavyoonekana kwa sasa;
Jay mwenyewe ambaye hadi wakati
tuliokuwa tunaongea naye alikuwa hafahamu kuhusiana na kutokea kwa issue
hii, amewaahidi mashabiki wake kulifuatilia swala hili na kuhakikisha
anaweka kila kitu katika mstari.
Rapa huyu mchana wa leo atakuwa
akitoa Burudani pande za Chuo kikuu Cha Dar es Salaam katika Kongamano
maarufu la Kigoda Cha Mwalimu Nyerere kwa mwaka huu, Kongamano ambalo
limeanza jana na linatarajiwa kuisha siku ya kesho likiwa na kauli mbiu
'Maendeleo ni Mapambano ya Ukombozi'.

Post a Comment