Header Ads

MTOTO WA MIEZI MIWILI ANAJISIWA


Tukio hilo limekuwa gumzo katika mitaa mbalimbali wilayani humo, huku baadhi ya wananchi wakidai kuwa linahusiana na imani za kishirikina.
Unaweza kujiuliza maswali mengi, hata inakuwaje mtoto wa miezi miwili kunajisiwa?
Katika vijiwe vya kahawa wilayani Mpwapwa, hii ni habari kubwa zilizokuwa zikizungumzwa   kuhusu kunajisiwa kwa mtoto huyo swali likibaki;  Je, yule mtu alimnajisi mtoto ameishia wapi?
Naingia chumba cha Mganga Mkuu Wilaya ya Mpwapwa kupata maelezo ya mtoto huyo tangu alipofikishwa katika hospitali ya wilaya hiyo, maendeleo yaliyofikiwa na utaratibu wa kiuchunguzi unavyoendelea.
Kauli ya Mganga Mkuu
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa, Lunemo Sakafu anasema kuwa tangu alipolazwa, mtoto huyo alikuwa akipelekwa kliniki kwa ajili ya kupatiwa chanzo mbalimbali na kupima afya yake, kwamba alikuwa na afya nzuri.
“Hakuzaliwa katika hospitali hii ila alikuwa akihudhuria kliniki, alizaliwa kwa wakunga wa jadi na mara ya mwisho kuja hapa hospitali ilikuwa Aprili 15, mwaka huu na alikuwa na afya nzuri,” alisema
Ashangazwa
Alisema kuwa alishangazwa na hali aliyokuwa nayo mtoto huyo alipofikishwa kwa mara nyingine katika hospitali hiyo kwani alikuwa akitokwa haja zote bila kikomo.
“Tunampatia matibabu ya kina ili kujua tatizo ni nini. Kwa sasa tuna utaratibu wa kumpeleka katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma ili akafanyiwe vipimo vya kina kwa kuwa mtoto huyu anatoa haja zote bila kikomo,” anasema  Sakafu.
Sakafu anasema hata wazazi wa mtoto huyo walipoulizwa juu ya hali aliyonayo mtoto wao, walipishana kauli katika maelezo yao na kwamba jambo hilo liliwatia shaka.               SOURCE.....MWANANCHI

No comments