GHOROFA LILILO KARIBU NA IKULU LAZUA UTATA
Inadaiwa kuwa, kwa kawaida serikali hairuhusu kujenga majengo marefu umbali wa mita mia kutoka ikulu. Jengo hilo linadaiwa kujengwa ndani ya mita 100 kutoka ikulu
WALIOPONZWA NA KUTOA KIBALI CHA UJENZI
Jumatano iliyopita, Mtendaji Mkuu na Msanifu Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar wakikabiliwa na mashitaka ya matumizi mabaya ya madaraka kwa kutoa vibali hivyo.

Maofisa
hao ni Makumba Kimweri (Mtendaji Mkuu) na Richard Maliyaga (Msanifu
Mkuu) walifikishwa kortini hapo na kusomewa mashitaka yanayowakabili na
Wakili wa Serikali, Leonard Swai mbele ya hakimu mkazi wa mahakama hiyo,
Sundi Fimbo.
Swai
alidai mahakamani hapo kuwa Agosti 6, 2007 Kimweri akiwa Mtendaji Mkuu
wa TBA kwa kutumia vibaya madaraka yake alisaini hati ya makubaliano
yenye namba TBA/JVA/DSM/ROI/001 kati ya TBA na Kampuni ya Royalle
Orchard Inn Ltd akiwa na lengo la kuanzisha ujenzi na wamiliki binafsi
wa umma wa ghorofa 15 kwenye Kitalu namba 45 Mtaa wa Chimara, Wilaya ya
Ilala bila eneo hilo kufanyiwa upembuzi yakinifu.
WENGI WALIKUWA WAKIJIULIZA KABLA YA WAHUSIKA KUSHTAKIWA
Upo ushahidi mkubwa kwamba, hata kabla ya Takukuru kuchukua hatua hiyo, wakazi wa Jiji la Dar waliokuwa wakupita eneo hilo, swali lao kubwa lilikuwa: Hivi ni kwa nini jengo refu kama hilo limejengwa jirani na ikulu?

Swali hilo lilikosa majibu hadi Jumatano iliyopita ambapo Takukuru iliwafikisha kortini maofisa hao wa TBA.
Post a Comment