Majeshi ya serikali ya Kongo yafanikiwa kudhibiti ngome ya waasi wa M23 karibu na mji wa Goma.
Majeshi ya
serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yamedhibiti maeneo ya
vilima vilivyopo karibu na mji wa Goma Mashariki mwa nchi hiyo, baada ya
wapiganaji wa kundi la waasi wa M23 kuondoka eneo hilo.
Waasi wa kundi
la M23 wamesema wameondoka eneo hilo la milimani ili kuruhusu uchunguzi
huru juu ya mashambulizi ya makombora yaliyosababisha vifo vya raia
mjini Goma na katika nchi jirani ya Rwanda.
Rwanda
imeishutumu Kongo kwa kufanya mashambulizi hayo kwa makusudi na kuibua
wasiwasi kuwa huenda kukawa na makabiliano kati ya nchi hizo mbili.
Wanadiplomasia
wa kanda ya maziwa makuu wamesema majeshi ya Rwanda yameonekana
yakisafiri kutoka mji mkuu kuelekea kaskazini mwa nchi hiyo.
Post a Comment