ANGALIA MTOTO WA BAKHRESA ALIVYOFANYA KUFURU DAR KWA KUJENGA BARABARA NA KUWEKA TAA HADI KWENYE MJENGO WAKE WA KIFAHARI
KAWAIDA wanasiasa ndiyo wamekuwa watu wenye ahadi nyingi sana linapofika suala la maendeleo kwa jamii.
Mara nyingi wamekuwa wakieleza namna wanavyoweza kuwapatia manufaa
wananchi kama watawachagua, mfano kuhakikisha wanapata maji safi,
barabara bora na vinginevyo.
Wanasiasa wanajulikana kwa kutotekeleza ahadi zao na wengi wao wamekuwa
wakishindwa kuzitekeleza kwa kutoonekana kabisa baada ya kupewa kura.
Halafu, wanaonekana kipindi kama hiki cha uchaguzi kwa kuwa kwa mara nyingine wanataka kupata kura, yaani wachaguliwe tena.
Kabla ya uchaguzi mkuu ambao unatarajia kufanyika Oktoba, mwaka huu,
huenda wanasiasa wanaweza kujifunza kupitia Yusuf Said Bakhresa.
Yusuf ambaye ni mmoja wa wamiliki wa klabu ya Azam FC na Azam Media
Group inayomiliki Azam TV, ameamua kumwaga takribani Sh milioni 400 kwa
ajili ya ujenzi wa barabara jijini Dar es Salaam.
Yusuf ambaye ni wakala wa kuuza wachezaji anayetambuliwa na Shirikisho
la Soka la Kimataifa (Fifa), tayari ameishajenga mitaa miwili na
anatarajia kujenga mingine miwili.
Mitaa yote ipo katika eneo la Msasani jijini Dar es Salaam, karibu
kabisa na yalipokuwa makazi ya hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere.
Ujenzi wa barabara hizo umefanywa na wataalamu wa Kichina ambao badala
ya kutumia lami kama ilivyozoeleka, Wachina hao wamejenga kwa kutumia
saruji, wakitupia zege lenye unene mithili ya mikate mitatu iliyobebana!
Ujenzi huo umeanzia kwenye mtaa unaotokea katika barabara ya Mwai
Kibaki, unaingia hadi kwenda kukutana na mtaa uliopewa jina la Ngome
Road.
Mtaa huo ndiyo kuna makazi ya milionea huyo upande mmoja akiwa amepakana
na kampuni maarufu ya upangishaji nyumba za kisasa ya Blue Mark.
Pamoja na kutengenezwa kwa ubora wa hali ya juu, milionea huyo
amehakikisha mitaa hiyo miwili imewekewa taa na ing’ara kama New York.
Huenda ndiyo mitaa miwili pekee inayoingia kutoka barabara kubwa yenye
taa nyingi kuliko yoyote ile jijini Dar es Salaam na Tanzania nzima.
Taa zake pia huenda ndiyo ghali kuliko zote zilizo katika mitaa ya jiji
la Dar es Salaam kwa kuwa zinatumia mfumo wa solar, hazitegemei umeme wa
Tanesco ambao hauna uhakika, maana unaweza kukatika wakati wowote.
Kama hiyo haitoshi, imeelezwa bajeti hiyo ya Sh milioni 400 itatumika
kuitengeneza mitaa mingine miwili ya Barakani Road na mwingine mdogo
unaounganisha Barakani Road na Ngome Road.
Ingawa wanaoishi katika maeneo hayo wengi ni vigogo, imeelezwa Yusuf
aliwachangisha kiasi kidogo cha fedha ambacho huenda hakifiki hata
asilimia 20 ya alichotoa.
“Alichofanya ni kama kutaka kuonyesha ujirani, yaani ajue anashirikiana
na watu wanaoishi karibu yake. Lakini fedha zote anatoa yeye na hatua ya
pili ni kujenga tena mitaa hiyo miwili,” alieleza rafiki wa karibu wa
Yusuf ambaye ni mmoja wa watoto wa bilionea namba moja Tanzania na
Afrika Mashariki, Said Salim Bakhresa.
GETI LA KUINGIA NYUMBANI KWAKE
Juhudi za kumpata Yusuf alizungumzie suala hilo zilikwama baada ya kuelezwa yuko safarini nje ya nchi kikazi.
Lakini taarifa za uhakika zinaeleza, hana mpango wa kugombea udiwani
wala ubunge, badala yake alifanya hivyo kama mchango wake kwa jamii na
kuboresha mazingira ya eneo hilo analoishi pamoja na majirani zake.
JUMBA LAKE LA KISASA NA KIFAHARI ANALOISHI....
Post a Comment