DAR LIVE IDDI MOSI, MADEE, NATURE, MZEE YUSUF KUWASHA MOTO
Hamad Ally' Madee'
WAFALME kunako Hip Hop na Taarab, Hamad Ally ‘Madee’, Juma Kassim ‘Nature’
pamoja na Mzee Yusuf wanatarajiwa kuangusha bonge la shoo Idd Mosi hii
ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem
jijini Dar.
Juma Nature.
Mastaa hao walizungumza na Uwazi Mizengwe
kuhusiana na shoo hiyo ambapo kila mmoja aliahidi kufanya makubwa
ambayo hayajawahi kutokea katika tasnia ya muziki huku wengine wakiahidi
kuachia nyimbo mpya.
Mja pani Mweusi
Pazia la burudani kwa watoto
litafunguliwa na mkali wa sarakasi Bongo anayekubalika nchini Ujerumani
na Australia, Ramadhan Adam ‘Mjapani Mweusi’ ambapo Idd Mosi hii
atafanya maajabu ya kihistoria.
“Watoto watafurahia tena sana sikukuu
hii kwani nitaingia na joka kubwa linaloitwa Anakonda ambapo kila
atakayetaka kulishika na kucheza nalo ataruhusiwa kwani halina madhara
yoyote. Pia nitakuwa na Dogo Kadogonda ambapo naye ataonesha maajabu ya
kujilipua kwa moto na kugaragara huku moto ukimuunguza,” alisema Mjapani
Mweusi.
Wakali Dancers.
Wakali Dancers na Masai Warriors
Mbali na Mjapani Mweusi, burudani Idd
Mosi hii itawashwa pia na wasanii tishio kwa kucheza na watoto, Wakali
Dancers pamoja na Masai Warriors ambapo siku hiyo watawachezesha watoto
michezo mbalimbali kwa staili kibao sambamba na mazingaombwe.
“Kila mtoto atakayefika atafurahi na
sisi kwani tutamfundisha jinsi ya kucheza muziki kwa staili tofauti na
watakaocheza vizuri watapata zawadi kutoka kwa Wakali Dancers,” alisema
mmoja wa mastaa wa Kundi la Wakali.
Siku hiyo Dar Live, watoto watacheza
michezo ya kuteleza, kubembea, kupanda ndege, mashindano ya kuogelea na
motto atakayependeza zaidi ya wenzake atapewa zawadi nono.
Madee
Shoo ya kibabe itaanzia saa moja usiku,
ambapo Rais wa Manzese, Madee atatinga na kundi lake la Tip Top
Connection kunukisha mwanzo mwisho.
“Mara ya kwanza kupiga shoo Dar Live
ilikuwa siku ya uzinduzi wa ukumbi huu miaka kadhaa iliyopita na ilikuwa
historia. Idd Mosi hii narudi kwa kishindo nikiwa Madee mpya na ngoma
mpya.
Mashabiki watarajie kusikia ngoma zangu
zote mpya kama vile Pombe Yangu, Ni Sheeda, Tema Mate Tuwachape na kwa
mara ya kwanza nitauzindua wimbo wangu mpya kabisa, mbichiiii ndani ya
Dar Live uitwao Kombe,” alisema Madee.
Nature
Mbali ya Rais wa Manzese, rais mwingine
kutoka Temeke na mkongwe mwenye miaka zaidi ya 16 kwenye muziki wa Bongo
Fleva, Nature naye atakuwepo sambamba na kundi lake la TMK Wanaume
Halisi. “Kama jana, kama juzi, kama kesho, wananiita Kibra ndani ya Dar
Live tukutane Idd Mosi hii kwani nitawasha moto wa aina yake.
Sina maneno mengi ila mashabiki wangu
wananitambua kwa vitendo kuanzia ngoma zote za zamani hadi sasa ni full
kuserereka,” alisema Nature.
Mzee Yusuf.
Mzee Yusuf
Ukiachana na wakali wa Hip Hop, usiku
huo utasimamiwa pia na kundi linalotikisa Bongo kunako miondoko ya
Pwani, Jahazi Modern Taarab likiongozwa na Mfalme Mzee Yusuf. “Baada ya
kukinukisha na tuzo zangu za Kili mwaka huu kwenye shoo ya Vunja Jungu,
niwaahidi mashabiki wangu, wapenda Taarab wote waje wamuone mbunge
mtarajiwa wa Unguja nikizindua Wimbo wa Kaning’ang’ania Ng’ang’ani na
nyingine kibao. Tutapiga nyimbo zote tisa zilizopo kwenye albamu yetu
mpya ya Mahaba Niue kama vile Nina Moyo Sina Jiwe wa Leila Rashid,
Siumbuki wa Fatma, Nia Safi Hairogwi wa Mishi na nyingine kibao. Kifupi
hatuna maneno mengi bali muziki wetu kila anayetuona jukwaani anajua
habari yake inakuwaje,” alisema Mzee Yusuf.
Msaga Sumu.
Msaga Sumu
Ukiachana na wakali wa Hip Hop na
Taarab, mfalme wa nyimbo za Singeli ambaye hana mshindani Bongo, Seleman
Jabir ‘Msaga Sumu’ naye atakuwepo kuwaburudisha mashabiki wote wa
kiswazi na kishua.
“Bila chenga muziki wangu hakuna
asiyeujua ni mperampera mwanzo mwisho. Naanza na Historia ya Kweli,
Rafiki wa Kweli, Huyo Mtoto, Napenda Simba na nyingine nyingi bila
kusahau siku hiyo kwa mara ya kwanza nitatambulisha ngoma yangu mpya
niliyoshirikiana na Nature inayoitwa Inaniuma Sana (remix),” alisema
Msaga Sumu.
Pam D.
Pam D
Staa wa Wimbo wa Nimempata anayesumbua
vichwa vya mastaa wa muziki wengi wa kike, Pamela Daffa ‘Pam D’ atakuwa
miongoni mwa wakali watakaotikisa.

Post a Comment