Header Ads

MAISHA BASEMENT: Burudani zitakuwa zikianza JUMATATU mpaka JUMATATU, soma zaidi hapa

IMG_20150714_094408
Maisha Basement zamani ilikuwa ikiitwa NEW MAISHA CLUB kwa sasa imehamia Makumbusho Kijitonyama jengo jipya la LAPF TOWERS. Club hii ni mpya na ya kisasa yenye uwezo wa kuchukua watu mia saba (700) yenye vifaa vya kisasa na dance floor ya kisasa yenye uwezo wa kurusha matukio live kama video na mechi za mpira.
Uzinduzi wa Maisha Basement utafanyika kwa siku 3 tofauti, uzinduzi wa kwanza utakuwa Jumatano ya tarehe 15.07.15 ambapo tutazindua na watu maarufu mbalimbali, na uzinduzi wa pili utakuwa Alhamis ya 16.07.15 na siku hii tutawaalika watu mbalimbali kutoka katika makampuni (Corporate People).
Na uzinduzi rasmi wa MAISHA BASEMENT utakuwa siku ya EID MOSI, ambapo tutakuwa na burudani mbalimbali, na mgeni rasmi atakuwa ni mkuu wa wilaya ya KINONDONI Mh PAUL MAKONDA. Siku hii kiingilio ni shiling elfu 10 tu. Burudani zetu zilikuwa zinaanza Jumatano mpaka Jumapili, lakini hapa Maisha Basement burudani zetu zitaanza Jumatatu mpaka Jumatatu.
IMG_20150714_094525IMG_20150714_095034IMG_20150714_095103IMG_20150714_095432
IMG_20150714_100546

No comments