Vanessa na Mzee Yusuf wakifanya yao.
Khadija Kopa akikamua sambamba na kundi zima la Ogopa Kopa.
Msanii wa Komedi, Zimwi akiwasalimia mashabiki.
Wasanii wa Bongo Muvi, Niva, Baga, Clayton wakiyarudi mangoma.
Waimbaji wa Kundi la Jahazi wakiwa tayari kufanya yao.
QS Mhonda akizindua albamu kwa kufungua box.
Hapa akionesha albamu hiyo.
Msanii wa Bongo Muvi, Gabo akiwasalimia mashabiki.
Mzee Yusuf akionesha ufundi wa kupiga kinanda.
Hapa akionesha ufundi wa kupiga gitaa.
Akikamua moja ya nyimbo za albamu hiyo na madansa wake.
Mtangazaji wa kipindi cha Taarabu, Mwanne akigawa keki stejini kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.
Nyomi ya mashabiki waliofurika ukumbini.
Mfalme wa Taarabu, Mzee Yusuf na mrembo anayetamba kwenye Muziki wa
Bongo Fleva kwa sasa, Vanessa Mdee wameweka historia ndani ya Uwanja wa
Taifa wa Burudani, Dar Live, usiku wa jana baada ya kuachia bonge la
shoo ya wimbo wao unaokwenda kwa jina la Mashallah.
Wawili hao walifanya shoo hiyo kwenye hafla ya uzinduzi wa albamu ya
kumi na moja ya Jahazi yenye nyimbo saba inayokwenda kwa jina la
Kaning’ang’ania huku wakisindikizwa na Kundi la Taarabu la Ogopa Kopa
linaloongozwa na Malkia Khadija Kopa.
Vanessa Mdee aliyepanda jukwaani na Mzee Yusuf sambamba na kundi zima
la Jahazi walipiga shoo ya kufa mtu na kuwaacha mashabiki wa muziki huo
vinywa wazi kwa mara ya kwanza wakishuhudia ladha ya muziki tofauti
kutoka kwa wawili hao.
Picha/Chande Abdallah na Boniphace Ngumije GPL
Post a Comment