Ndege ya askari wa doria yatunguliwa na majangili

Kwa
mara ya kwanza katika historia ya uhifadhi nchini majangili wa tembo
wametungua chopa ya askari wa doria iliyokuwa ikimilikiwa na mwekezaji
wa kitalu cha mwiba holdings katika pori la tengefu la maswa mkoani
wilayani meatu mkoani simiyu na kusababisha kifo cha rubani wa chopa
hiyo huku rubani mwenzie akijeruhiwa vibaya mguuni Chopa hiyo
inasemekana ilitunguliwa majira ya saa kumi na mbili jioni jana na
Majaangili hao ambao wanaosadikika kutumia silaha nzito za kivita
walifanikisha kutekeleza uhalifu huo walipo gundua kuwa chopa hiyo
ilikuwa ikiwafuatilia baada ya kubaini mahali walipo na uhalifu
waliokuwa wakiutekeleza katika pori hilo,ambapo inaripotiwa kwamba
pamoja na kutungua chopa hiyo walisha fanikiwa kuuwa tembo watatu
Post a Comment