Jerry Muro: 'Simba si Washindani Wetu Tena...Watabaki Kuwa Watani Wetu Kama Wagogo na Wasukuma'

Klabu ya soka ya Yanga imetangaza rasmi kuwa kuanzia leo wekundu wa
Msimbazi Simba si washindani wao tena bali ni watani wa jadi kama
walivyo wasukuma na wagogo.
Aidha Muro ameongeza kuwa kwa sasa wanachotazama ni shughuli tatu zilizo
mbele yao mechi ya kombe la shirikisho dhidi ya JKT Mlale, mchezo wa
klabu bingwa barani Afrika dhidi ya Cercke de Joachim ya Mauritius na
mechi dhidi ya Azam ikiwa ni ya ligi kuu Tanzania bara.
Aidha amesema kuwa kikosi cha Yanga kimeanza mazoezi katika uwanja wa
chuo cha polisi Kurasini kwa ajili ya mchezo wa kombe la shirikisho
dhidi ya JKT Mlale Jumatano na mara baada ya mchezo huo kitaendelea na
maandalizi ya mechi ya marudiano dhidi ya Cercle de Joachim.
Post a Comment