Zanzibar: Mwandishi wa Habari wa Radio Deutsche Welle(DW-Swahili), Salma Said Akamatwa na Haijulikani Alipo......Hapa Kuna Mahojiano Akiwa Kusikojulikana
Mwandishi wa Habari wa Radio Deutsche Welle(DW-Swahili), Salma Said jana
alikamatwa na watu wasiojulikana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Abeid Amani Karume mjini Unguja, alipokuwa akisafiri kwenda Dar es
Salaam kwa ajili ya kuangalia afya yake.
Akizungumzia tukio hilo jana, mume wa Salma, Ali Salim Khamis ambaye pia
ni Mbunge wa Mwanakwerekwe (CUF), alisema alipata ujumbe wa maandishi
kutoka kwa mkewe kwamba amekamatwa.
Khamis alisema alipokwenda uwanja wa ndege aliambiwa na mkuu wa polisi
wa uwanjani hapo kwamba hana taarifa za tukio hilo jibu ambalo alilipata
pia kwa Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Mjini Magharibi.
Alisema aliamua kwenda kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa ambako pia
aliambiwa hawana taarifa za kukamatwa kwa Salma. “Hadi sasa sijui mke
wangu yuko wapi bado naendelea kumtafuta.”
Khamis alisema Salma alikuwa tayari amepitia taratibu zote na alikuwa
akisubiri kuingia ndani ya ndege ambayo haikutajwa, lakini alisema ndege
hiyo iliyokuwa iondoke saa 8.05 mchana ilizuiwa na watu hao wanaodaiwa
kuwa ni askari hadi saa tisa kasoro, walipoiruhusu lakini ikidaiwa kuwa
waliondoka na Salma kwenda kusikojulikana.
Post a Comment