Nick wa Pili Akanusha Kumwandikia Joh Makini Mashairi
Joh Makini aliongelea issue kuwa kuna watu wanadhani yeye huandikiwa mashairi na mdogo wake Nick wa Pili kwenye ngoma yake Don’t Bother.
Na sasa Nick amezungumzia jambo hilo analolielezea kama ni propaganda. Amesema Joh alianza kuhit na nyimbo kibao kama Chochote Popote na album ya Zamu Yangu kipindi ambacho hakuna alikuwa akimfahamu yeye na alikuwa hawezi kuandika kama kaka yake.
“Sijui ni nani alianzisha hiyo propaganda, ni kama hiyo propaganda ya kuwa Weusi wanabebwa. Ni rahisi sana kusema Weusi wanabebwa, ni ngumu sana kusema Don’t Bother wanabebwa, ngumu kusema Baba Swalehe anabebwa lakini unaposema Weusi unakuwa unabebwa ukweli,” Nick aliiambia 255 ya XXL kupitia Clouds FM.
Post a Comment