Zile Sauti za Kimahaba Mtandaoni za Wema na Mbowe, Kumbe Mchezo Mzima Hivi Ndivyo Ilivyokuwa A- Z
Siku
chache baada ya kusambaa kwa sauti katika mitandao ya kijamii, ikiwemo
WhatApp na Facebook, inayodaiwa kutengenezwa kwa lengo la kumchafua
Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe na mrembo wa
Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu, hatimaye ‘dude’ limeamka na sasa
kimenuka.
HAPA NDIPO ILIPOANZIA
Mwishoni
mwa wiki iliyopita, sauti iliyorekodiwa kama ya watu wanaoongea kwenye
simu, zilianza kusambaa kwa kasi mitandaoni, ambazo kwa kuzisikia
harakaharaka, zilionekana kufanana na watu hao wawili, zikisikika kama
za watu waliokuwa katika uhusiano.
Wakati
sauti hizo zinasambaa, muda mchache baadaye, majibizano ya meseji
kwenye simu yakaanza kusambaa pia, ambayo nayo yanahisiwa kuwa
yalitengenezwa, yakiwahusisha viongozi wawili wa ngazi za juu katika
Mikoa ya Arusha na Dar es Salaam, wakipongezana kwa kukamilika vizuri
kwa kazi hiyo (ya kutenegeneza na kusambaza sauti). Katika majibizano
hayo ya meseji za simu, ‘viongozi’ hao wawili walimsifu mtu waliyemwita
Steve (anadhaniwa kuwa Steve Nyerere) kwa kuifanya kazi hiyo vizuri (ya
kuigiza sauti ya kiongozi huyo).
RISASI LAWASAKA WAHUSIKA
Ili
kupata mkanda kamili wa ishu hiyo, Risasi Mchanganyiko liliingia mtaani
na kuifanyia kazi ili liweze kuwapa wasomaji wake kitu cha kueleweka.
Freeman Alkael Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema Taifa,
hakupokea simu aliyopigiwa, lakini wakati Risasi Mchanganyiko likienda
mitamboni, alisikika kupitia kituo kimoja cha redio jijini Arusha,
akiikana sauti hiyo na kusisitiza kuwa hajawahi kuwa na uhusiano wa
kimapenzi na muigizaji huyo na kwamba kinachofanyika ni siasa chafu,
kitu ambacho kitashughulikiwa na chama.
Wema
Sepetu naye simu yake iliita bila kupokelewa na hata baada ya kutumiwa
ujumbe mfupi, hakujibu licha ya kuonekana kuwa umepokelewa na kusomwa.
HUYU HAPA MLEZI WA WEMA CHADEMA
Hata
hivyo, Risasi Mchanganyiko lilifanikiwa kumpata mtu aliyepewa jukumu la
kumlea Wema ndani ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),
Boniphace Jacob ambaye pia ni Meya wa Ubungo jijini Dar es Salaam na
hapa anafunguka kuhusu ishu hiyo; “Tumeshaongea na wanasheria juu ya
hatua kali za kisheria, kuwachukulia hatua
wote
wanaoigiza sauti za viongozi wetu na kuzitumia vibaya kwa nia ya
kuwadhalilisha na kuwashushia heshima, pamoja na kutoa taarifa kwenye
vyombo vya dola juu ya uchunguzi ufanyike kubaini sehemu na watu
wanaofanya “voice studio” kwa lengo ovu.
“Pili
tumemtia moyo kamanda wetu Wema kuwa asihofu na siasa za majitaka na
kwamba yote yanafanyika na wapinzani wetu, kwa sababu wanamuhofia na
kumuogopa
juu ya namna anavyofanya mikakati ya kufuta
“UTUMWA WA WASANII KWA CCM”
kazi ambayo ameifanya na mpaka sasa ameandaa ujio wa wasanii wakubwa 20 ndiyo maana wanataka kumuondoa nje ya agenda yake.”
STEVE NYERERE NAYE AFUNGUKA
Steve
Nyerere ambaye kwa mujibu wa meseji zilizoenezwa mtandaoni alionekana
kama ndiye aliyeshughulika kutengeneza sauti hiyo ya kiume, aliruka
kimanga kuhusika na suala hilo, aliloliita la kijinga na kipumbavu.
“Mimi sihusiki, sikutengeneza ile sauti kwa vile sina sababu ya kufanya
hivyo,
hicho
ndicho ninachoweza kukuambia ila kwa nyongeza tu, niwatake Watanzania
waachane na kufuatilia mambo ya kijinga na kipumbavu, tuna vitu vingi
sana vya kufanya badala ya kukuza vitu kama hivi.”
SASHA NAYE AZUNGUMZIA ‘SAUTI YAKE’
Sasha, msanii ambaye hutumika kama video queen kwenye nyimbo mbalimbali za Bongo Fleva, ambaye
amefanana
sauti kwa kiasi kikubwa na Wema Sepetu, anahusishwa kutumika
kutengeneza sauti ya kumuigiza malkia huyo wa filamu Bongo. “Nimetumika
kuiga sauti ya Wema? Hapana, sijawahi kupigiwa simu na mtu yeyote na
wala sijafanya kitu kama hicho, nikuambie ukweli kuwa hili jambo ndiyo
kwanza wewe unaniambia, sijui kabisa,” alisema msanii huyo.
TUNDU LISU ABEZA
Mwanasheria
Mkuu wa Chadema, Tundu Lisu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki,
alipotakiwa kulizungumzia suala hilo, alisema ni propaganda dhaifu,
zilizolenga kumchafua mwenyekiti wao, ambayo imeshindwa. “Lengo lao
lilikuwa ni kumchafua mwenyekiti wetu, lakini hawajaweza kwa sababu
hawezi kuchafuka kwa staili hii. Tunajua hili jambo hata tukilipeleka
polisi ni kama kujisumbua tu, hawana historia ya kushughulikia shida za
wapinzani.”
HAWA HAPA POLISI MAKOSA YA MTANDAO.
Risasi
Mchanganyiko lilimpata mmoja wa maofisa wa kitengo cha makosa ya
mtandao, ambaye alijitambulisha kwa jina moja la Fadhil, akisema yeye
siyo msemaji wa suala hilo. “Ila ninachoweza kukusaidia kwa hili ni
kwamba Cyber Crime haifanyi kazi pasipo kupokea malalamiko. Hao ambao
sauti zao unasema zimeigwa, wanatakiwa waje kulalamika hapa na hapo
ndipo polisi watakapoanza kufuatilia suala hilo. “Lakini kama wenyewe
watakaa kimya bila kulalamika, basi suala hilo litaishia kama lilivyo,
endapo watakuja suala hilo litafanyiwa kazi mara moja,” alisema.

Post a Comment