FACEBOOK YASABABISHA MAGONJWA MAPYA YA KIDIJITALI SOMA HAPA BY CHEKA NA KITIME
Kutokana na matumizi
makubwa ya Facebook tayari kumeanza kupatikana magonjwa ambayo yanatokana na
hii kitu, katika semina niliyohudhuria jana niliweza kufahamishwa baadhi ya
magonjwa mapya kabisa yafuatayo;
1.LIKOSIS.
Huu ni ugonjwa ambao
mgonjwa huwa ana ‘like’ kila status na picha yoyote atakayoiona mbele yake. Ugonjwa
huu huwapata hasa wale ambao ndio kwanza wanaanza kutumia FB
2.LIKOPHOBIA
Huu ni ugonjwa wa kutoku
‘like’ kitu chochote, ugonjwa huu wanao sana masupastaa wa bongo, maana huwa na
tatizo la kisaikolojia kuwa waki’like’ watashuka hadhi na kuwa watu wa kawaida
3.AIBUMIASIS
Huu ni ugonjwa wa kuionea
aibu FB. Mtumiaji huingia FB labda mara moja kwa mwezi halafu anaona aibu
kuingia tena mpaka mwezi unaofuata.
4. TAG SYNDROME
Ni ugonjwa ambao mwana FB
anataka umtag kila picha anayoiona hata isiyomuhusu
5. HATE SYNDROME
Huu ni ule ugonjwa wa mwana
FB ambapo yeye huweka status za ‘hate’ tu. I hate life. I hate haters, I hate
Dar, I hate CCM, I hate CDM
6. REQUEST SYNDROME
Hapa ni ule ugonjwa wa
mwana FB kurequest marafiki bila hata kuwa anawajua anataka tu aonekane anao
wengi.
7. COMMENTOLARIA
Mwenye ugonjwa huu, hu
comment kwenye kila status itakayotokea mbele yake, yanayomhusu na yasiyomhusu, mradi ka comment
8.MBULULATOSIS
Mwenye
ugonjwa huu hucomment utumbo tu kila mara, status na mazungumzo
yanaweza kuwa ni ya kuhusu ujio wa Obama, yeye ataweka tangazo la duka
lake la simu, au ataulizia Kofi Olomide ana umri gani
9. ADICTOMIOLOGY
Mgonjwa anaweza kuhisi kufa
kama katimiza masaa 24 bila kuingia FB
Post a Comment