Kampeni CCM: Naibu Spika,Job Ndugai ampiga mgombea mwenzake, azimia na kukimbizwa hospitali huko Kongwa
Hatimaye Mheshimiwa Ndugai amechimbia kaburi la kisiasa baada ya
kumshambulia Mgombea mwenzake aitwae Dr Joseph Elieza Chilongani kwa
gongo katika mkutano wa kuomba kupigiwa kura za maoni CCM
Hayo yametokea leo mnamo saa saa 10 jioni katika kitongoji cha ugogoni mjini Kongwa.
Katika kile kinachoonekana ni kuishiwa sera na kutumia ubabe na ukorofi
ili kutetea nafasi yake ya kugombea ubunge wa Jimbo la Kongwa,
Mheshimiwa Naibu Spika wa Bunge La Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
Mbunge wa Jimbo la Kongwa alipiga kwa gongo ambalo amekuwa akitembea
nalo huku wasimamizi wa uchaguzi wakifumbua macho kitendo cha mgombea
kutembea na silaha hiyo kwenye kampeni.
Inadaiwa na mtu aliyefuatilia kwa karibu tukio hilo mkutanoni kuwa Kuna
mgombea mmojawapo (mkazi wa Kongwa aitwaye ngatunga) Alisimama kuuza
sera zake na kudai kuwa Kongwa kuna madini jimbo halijafaidika na
chochote kutoka kwa wachimbaji wa madini... Mara moja Ndugai alimtishia
kuwa anyamaze la sivyo angemuonesha kazi kwa kile anachodai kuwa ni
kuongea upuuzi..
Wakati wagombea hao wakiendelea kujibizana suala hilo ndipo ghafla
mheshimiwa alipomuona Mmojawapo wa wagombea aitwaye Dr Joseph Chilongani
ameshika simu na kutahamaki kuwa alikuwa akimrekodi kwa kuvunja
taratibu.
Ndipo Job Ndugai alipoamka na kumwambia "Tena wewe nilikuwa nakutafuta
siku nyingi sana, unanirekodi na makamera yako na leo utanitambua mimi
ni nani."
Mara Ndugai akakusanya nguvu na kumpiga Dr Chilongani kwa fimbo hiyo.
aidha hata baada ya kuanguka chini Ndugai alimfuata na kumrukia
kumkanyaga tumboni akiwa na hasira na nia ovu ya kutaka kumdhuru zaidi..
Baadae wananchi walipata hasira na kutaka kumshughukilia kwa kichapo
Mbunge huyo na ndipo alipopanda haraka gari lake haraka na kukimbi Eneo
la Tukio..Inasadikiwa yule mgombea mwingine alijaribu kumnyanyua Dr.
Pale chini, jambo ambalo baadhi ya wananchi walilichukulia ni kama
kutaka kumdhuru zaidi hivyo walianza kumpa kichapo huyo mgombea mwengine
kiasi hadi watu wengine walipoamulia.. Baada ya tukio hilo ovu mkutano
ulivurugika.
Ndugu zake Dr. Chilongani kwa kusaidiana na watu walimbeba akiwa amezimia na kumkimbiz hospital baada y kupata PF 3 toka polisi.
Hadi reporter anaondoka hospitalini Dr alikuwa bado hajazinduka na
madaktari walikuwa wanaendelea na harakati za kuokoa maisha ya mgombea
huyo.
Shuhuda mmoja wa tukio anasema kuwa tukio hilo lilirekodiwa na pengine
ushahidi huo utatumika katika kumuengua Ndugai katika kinyanganyiro cha
ugombea ubunge kwa ticket ya CCM hasa baada ya watia wengine kuweka
pingamizi mara mbili lakini bado uongozi wa chama ulikuwa unafumbia
macho.
Baadhi ya wanachama wa CCM walidai kuwa kama haki itatendeka Ndugai
atakuwa amejichimbia kaburi la kisiasa na kushuhudia KIAMA CHAKE RASMI
KATIKA SIASA ZA JIMBO LA KONGWA..
Post a Comment