Mgombea Ubunge CCM Aanguka Jukwaani Akiruka Kichurachura........Alitaka Kunogesha Mtindo wa CCM wa Push Up za Magufuli
Mgombea ubunge wa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)
katika jimbo la Tunduru Kaskazini,Mhandisi Ramo Makani alianguka
jukwaani wakati akijaribu kuruka kichura chura.
Tukio hilo lilitokea katika mkutano wa ufunguzi wa
kampeni za mgombea huyo, uliofanyika kwenye viwanja vya baraza
la Idd mjini hapa.
Inasadikiwa kuwa alikusudia kunogesha staili ya
mgombea urais wa tiketi ya CCM,Dr. John Magufuli ya kupiga Push
Up..
Ingawa tukio hilo lilionekana kumfedhehesha,mgombea
huyo alijikakamua kuinuka huku akisaidiwa na walinzi wake na
kuendelea kunadai sera zake.
Alisema kuwa katika kipindi kilichopita alitekeleza
ilani ya chama chake kwa kusimamia ujuenzi wa barabara ya
Namtumbo-Tunduru hadi wilayani Nanyumbu inayoendelea kujengwa kwa
kiwango cha lami.
Post a Comment