Hii Ndio Siri Ya Msanii Ray Kuwa Mweupe
Mwigizaji
maarufu wa Bongo Movie hapa nchini Ray Kigosi amesema kwamba yeye
hajawahi kujichubua bali huwa anakunywa maji mengi pamoja na kufanya
mazoezi .
Ray
ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano katika kipindi cha ENews
kinachorushwa na EATV na kusema kwamba hua anakwenda salon mara moja kwa
wiki kwa ajili ya kusafisha uso wake (Scrub) ili akiwa anafanya kazi
zake watu waweze kumwona vizuri na kupenda kazi zake.
Naye
Mpenzi wake Chuchu Hans amesema kwamba Mpenzi wake hajichubui bali ni
maisha yamemkubali tofauti na hapo nyuma alivyokuwa anahangaika kuinua
sanaa na kipaji chake.
Katika
kipengele cha ''Cheche'' ambacho majirani hupewa nafasi ya kumzungumzia
msanii au mgeni wa siku kwenye show wamesema kwamba Ray apunguze
kutumia vipodozi kwani anakuwa kama mchina.

Post a Comment