Lissu aumbuliwa vibaya bungeni

Ni baada ya kuomba Mwongozo kuhusu swala lililoleta utata kwa siku kadha
kuhusu uhalali wa serikali kuwasilisha mpango wa mwaka mmoja badala ya
miaka mitano.
Awali akiomba Mwongozo mh.Lissu alisema serikali imekiuka kuleta mpango
wa mwaka mmoja badala ya miaka mitano ambayo ndio desturi ya mabunge
yote yaliyopita na kumtaka Spika kutokubali kuruhusu bunge lake tukufu
kukiuka kanuni zake kwa faida ya serikali. Huku akiendelea na kibwagizo
cha hapa kazi tu hapa kazi tu.
Kwa kukazia ndipo akasimama Mh.Zitto na kuikumbusha serikali kuwa
serikali ilikuwa na uwezo kuwasilisha hoja ili kanuni zitenguliwe na
mpango wa mwaka moja ujadiliwe na kanuni zinaruhusu utenguaji huo.
Ndipo aliposimama Waziri na kusema kuhusu suala la utenguaji wa kanuni
serikali ilishakaa na kamati ya kanuni ambapo kiongozi wa KUB alishiriki
kwa kutuma mwakilishi, na Mwakilishi mwenyewe alikuwa Lissu.
Waziri akasema anamshangaa Lissu kwa kuomba mwongozo jambo ambalo
alishiriki kutoa maamuzi na akasema anaweza kutaja hata majina ya
wajumbe wote walioshiriki huo uamuzi.
NB. Wabunge waache unafiki na kuwa vigeugeu kwa kutafuta umaarufu usio na tija.
Post a Comment