Kutoka Mbeya, Mwanamke Ajigeuza Kunguru.....Polisi Wahaha Kumsaka

Mwanamke anayesadikiwa kuwa mshirikina na kukutwa na mali za wizi



Mali zinazosadikiwa kuwa za wizi zilizokamatwa

Jeshi la Polisi likiondoka na Mali zinazodhaniwa kuwa za wizi


Orodha ya mali iliyokamatwa
JESHI la Polisi Mkoa Mbeya limejikuta likitumia zaidi ya masaa manne
kumtafuta mtuhumiwa wa ushirikina bila mafanikio kutokana na mtu huyo
kujigeuza Kunguru.
Tukio hilo la ajabu lilitokea juzi kuanzia majira ya saa nne asubuhi
ambapo Jeshi la Polisi lililazimika kusaidiwa na wananchi kumkamata
Mwanamke mmoja aliyekuwa amejificha kiushirikina kwa kujigeuza kunguru
katika mtaa wa Mapelele kata ya Ilemi jijini Mbeya
Tukio hilo lilitokea baada ya polisi kufika nyumbani kwa mwanamke huyo
ambaye anatuhumiwa kumjeruhi vibaya jirani yake aitwaye Anitha Simon kwa
kipigo kwa madai ya kumuibia ndala jozi mbili aina ya yeboyebo.
Akizungumza katika eneo la tukio, mtoto wa kaka wa mtuhumiwa ambaye
ndiye aliyefanikisha zoezi la kumkamata ,Venance Mwalindile alidai yeye
ni chifu katika ukoo wao na kwamba anakerwa na tabia za shangazi yake
huyo.
“Nimeamua kufanya hivi kumuumbua shangazi kwani nimekerwa sana na hizi
tabia na ndiyo maana nimejitolea kuwasaidia polisi mkamata ili sheria
ichukue mkondo wake”alisema Mwalindile.
Hata hivyo Mwalindile alisema kuwa ilikuwa ni kazi ngumu kwake kumkamata
mama huyo anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka kati ya 45 hadi 50 kwani
akiwa amejificha chumbani alijibadilisha kuwa kunguru ambapo katika
mapambano makali alifanikiwa kumkamata na kumnyonga kunguru huyo ndipo
aliporudi katika hali yake ya kawaida na kuwakabidhi Polisi.
Akizungumzia tukio hilo ambalo lilijaza umati wa watu waliokuwa
wakishuhudia,Mwenyekiti wa mtaa jirani wa Mwafute Kata ya Ilemi, Charles
Kasyupa alisema kuwa wamekuwa na vikao vya mara kwa mara kuhusiana na
matukio ya wizi na ugomvi wa mtuhumiwa huyo lakini kumekuwa hakuna
mwafaka.
Baada ya kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo Polisi walifanya upekuzi
katika nyumba yake na kufaninikiwa kuvikuta vitu kadhaa vinavyodhaniwa
kuwa ni vya wizi vikiwemo Radio,magodoro,TV,madishi ya kuogea,viti vya
Kanisani,mafuta,sukari,spika za Kanisani,nguo mbalimbali na vitu vingine
ambavyo idadi na thamani yake haikuweza kufahamika mara moja.
Aidha baada ya kumaliza kupekua nyumba hiyo majira ya saa moja jioni kwa
hofu ya usalama wa wananchi waliokuwa na hasira kali Jeshi la Polisi
lililazimika kusomba mali zilizokutwa katika Nyumba ya mtuhumiwa.
Jeshi hilo lilitumia gari za Polisi aina ya Land cruser zilirudia mara
sita kubeba mali hiyo na kuipeleka Kituo Kikuu cha Polisi cha Kati kwa
ajili ya utambuzi wa mali hiyo wakiwa wameongozana na Mwenyekiti wa mtaa
wa Mapelele Jitihada Mwaijulu.
Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ahmed Msangi amekiri kukamatwa kwa
mwanamke huyo lakini Jeshi lake bado linaendelea na uchunguzi na atatoa
ufafanuzi baada ya kukamilika kwa uchunguzi wa tukio hilo.
Via>>Mbeya yetu blog
Post a Comment