Hatua 6 Za Kumzuzua Mwanamke Akupende Zaidi
Ukweli usemwe. Ndoto ya kila mwanaume katika hii dunia wakati mmoja au
mwingine hufikiria kuwa na kipawa cha kuweza kumzuzua mwanamke yeyote
anayemzimia. Uzuri ni kuwa hauhitaji kuwa tajiri ama kuvutia ili uwe na
kipawa kama hiki.
Kujifunza kuzuzua mwanamke si jambo kubwa vile, mwanzo ni rahisi zaidi
kwa mtu yeyote yule kutimiza jambo hili kama atafuata hatua
zinazohitajika kwa umakini.
Wengi wa wanaume wanashindwa kumzuzua mwanamke wa ndoto yake kwa sababu
wanatumia mbinu ambazo zimepitwa na wakati ama kutumia mitindo ambayo
haikubaliki.
Well, nimekuandalia hatua 6 za kufanya ili umzuzue mwanamke yeyote yule.
1. Pokea pongezi
Wanaume wengi wanatabia ya kukataa kupokea pongezi kutoka kwa mwanamke.
Balada ya wewe kuguna ama kutojiskia huru wakati mwanamke anakupongeza,
mbona usitumie nafasi hii kutumia maneno ya utamu kama ile 'asante,
'nashukuru' nk.
Kupokea pongezi kutoka kwa mwanamke ni kama vile kupokea zawadi kutoka
kwake, hivyo kufanya hivi kutakuwa kukimfurahisha mwanamke kila wakati.
2. Kuwa na maoni chanya kujihusu
Kama hujiamini wewe mwenyewe ama unajiona huwezi kutimiza kumfurahisha
mwanamke je unatarajia mwanamke akupende? Hivyo basi iwapo unataka
kumzuzua mwanamke unafaa ujiamini wewe mwenyewe kama mwanaume.
Njia rahisi ya kutimiza hii ni kuhakikisha unavalia nguo za kupendeza,
unavalia marashi yakunukia, na kuwa nadhifu. Wanawake wengi wanapenda
mtizamo aina hii.
3. Jifundishe kudensi
Ok wengi wangeuliza kwa nini nijifunze kudensi? Kudensi ina uhusiano wowote upi na kumzuzua mwanamke?
Jibu rahisi. Kwanza ni kuwa wanawake wanapenda sana wanaume ambao
wanajua kudensi. Hivi ushajiuliza kwa nini dancers wengi wanapendwa na
wanawake?
Pili ni kuwa wanawake wanaamini ya kuwa dancers wengi wanaujua mchezo ikija maswala ya chumbani.
Tatu ni kwa hautarajii mwanamke unayemzimia adensi na wanaume wengine wakati mumeenda kwa kilabu.
So ni muhimu kujifunza kudensi, atleast style moja mbili za kumdanganya.
4. Tumia jina lake
Siri nyingine ya kumzuzua mwanamke ni kumtaja jina lake wakati wa
maongezi. Kulingana na mwandishi maafuru wa kiingereza Dale Carnegie,
anadai ya kuwa sauti tamu zaidi kwa sikio la mwanamke ni kusikia ukitaja
jina lake.
Kama umekuwa ukifanya uchunguzi ni kuwa wengi wanahepa kutumia majina ya
wapenzi wao nk. Hivyo wewe usikubali kuanguka ndani ya hio kategoria.
Waonaje sasa uanze kutumia jina lake kila wakati unapomtext ama kuongea
naye? Amini usiamini jambo hili linafanya kazi kama uchawi.
5. Muangazie yeye
Iwapo unataka mwanamke akuchukie kwa siku moja basi ongea na kujisifu wewe mara kwa mara wakati mnapoongea pamoja.
Iwapo unataka kumzuzua mwanamke basi kinachohitajika ni kuhakikisha unampa atenshen yako yote wakati mko pamoja mnaongea.
6. Kuwa mcheshi
Imethibitishwa ya kuwa hakuna mtu angependwa kujihusisha na mtu
anayeboa. Hivyo kama unakipawa cha ucheshi ama unauwezo wa kumfanya
mwanamke avutiwe nawe basi hio ni silaha kubwa ya kumfanya mwanamke
azuzuike kwako.
Hitimisho: Matumizi ya mbinu hizi na sanaa nyingine za kutongoza
tulizichapisha awali zitaksaidia wewe pakubwa kuhakikisha ya kuwa
unamzuzua yeyote yule.

Post a Comment