Mapenzi ya Barakah Da Prince na Najma kimenuka...!
Kupitia U Heard ya XXL leo October 7, 2016 Mtangazaji Soudy Brown kutoka Clouds FM
amezungumza na kijana mmoja aliyejiita Rogers ambaye amedai ni mdogo wa
star wa hit single ya Nisamehe Barakah Da Prince na kueleza kuwa
mapenzi kati ya kaka yake na Najma hayako sawa.
Kwa mujibu
wa Rogers ameeleza kuwa Barakah Da Prince na Najma hawako poa kama
zamani baada ya kutokea kukosa maelewano kati yao na sababu ikitajwa
kuwa Najma ndiye tatizo kutokana na kutowapenda ndugu wa Barakah na
imeshatokea mpaka mama yake na Barah amekuwa akilalamika sana kuhusu
uhusiano huo.
>>>Kilichotokea
wiki iliyopita Najma alikuja na kuingia nyumbani kama saa 4 usiku mpaka
nikashtuka ameingiaje, alimkuta dada ambaye aliletwa na kaka akauliza
huyu ni nani? nikamwambia ni dada wa kazi ameletwa na kaka akingia
chumbani akakuta pochi ya kike akauliza ni ya nani nikasema ni ya dada
yetu akaitoa akaiweka chumbani kwangu.
Ikabidi
nimwambie kaka alikua kwenye Interview akaanza kunitukana akaanza
kunitukana kwanini Najma ameingia ndani, kwanini umemfungulia mlango
nikasema sio mimi akanambia mwambie kaka amesema harudi na hata akirudi
halali na wewe kwanza mtukane aondoke. Nikaenda chumbani kwao
nikamwambia mwambia kaka amesema harudi hapa na uondoke haraka, Najma
akakasirika akaondoka:- Rogers

Post a Comment