Mama Mzazi Wa Hamissa Mobetto Aiomba Familia Ya Diamond Msamaha.
Baada ya Matusi yanayoendelea mitandaoni kwa Hamisa Mobeto Kutoka katika familia ya Daimond na team Zari baada ya Daimond kurudiana na mzazi mwenzake Zari, Mama Mzazi wa mwanamitindo Hamisa Mobeto ameingilia kati ugomvi huo wa chini kwa chini unaoendelea mitandani kwa kumuombea mwanaye Msamaa.
Mama Mzazi wa Hamissa ameonekana kuumizwa na matusi na maneno anayotumiwa mwanaye na kuamua kuonyesha hisia zake kupitia ukurasa wake wa istargram kwa kuandika hivi;-
" Mmenitukania mwanangu hadi tumbo la uzazi limeniuma natamani ningewazaa wawili ili afarijiwe na mwenzie, pia ningeomba familia ya zote zilizo instagram mpunguzeni matusi na kumdhalilisha mwanangu kama kawakosea ninamwombea msamaha mwezi huu mtukufu.... mpeni amani ili na mimi nifurahie furaha ya uzazi wangu. Ni mwenyezi mungu pekee huchagua barabara atakayopitia mwanangu"


Post a Comment