Header Ads

TALK SHOW ZIARA NILIYOIFANYA KATIKA SHULE YA SEKONDARI YA MAKONGO, KUZUNGUMZIA NGONO ZA MAPEMA NA MATUMIZI YA MITANDAO YA KIJAMII

Superwoman nikiongea na wanafunzi wa shule ya Makongo
Hii ni ziara ambayo niliamua kuifanya katika harakati za kulijengea taifa hili vijana makini ambao tunategemea baadae kuwa viongozi watakaoliongoza taifa hili ipasavyo.
Nilipokuwa shule hii ya Makongo, niliweza kukutana na vijana wa vidato tofauti tofauti na kuzungumza nao juu ya masuala mazima ya matumizi ya Mitandao ya Kijamii 'Social Networks' mfano Facebook, Twitter, Instagram n.k; Pamoja na suala la Ngono katika umri mdogo.
Wanafunzi wakisalimia kwa adabu timu nzima ya 'Wanawake Live' iliyotembelea katika shule yao ikiongozwa na Joyce Kiria 
Mitandao ya kijamii imechukua sura tofauti hasa kwa upande wa vijana ambao wamekuwa wakiitumia tofauti na kujikuta wakijifunza vitu visivyo na msingi na kusahau kuwa mitandao hiyo ikitumiwa vizuri huleta maendeleo makubwa hasa kwa upande wa elimu na maisha kiujumla.
Niliweza kuwauliza baadhi ya wanafunzi jinsi gani wanatumia mitandao hiyo na nilijikuta nikipata majibu tofauti huku mengine yakiwa ya msingi ingawa sikuwa na uhakika kama ni kweli wanafunzi hao wanaitumia kama walivyonieleza.

Mmoja ya wanafunzi akichangia hoja husika
Suala la ngono katika umri mdogo pia lilichukua sura yake na niliweza kusikia maelezo tofauti kutoka kwa wanafunzi hao huku wengine wakifunguka ni jinsi gani wameweza kukumbana na matatizo hayo na jinsi gani waliweza kujiepusha na kutojihusisha na ngono katika umri huo mdogo.
Nikiteta jambo na mabinti hawa wa shule ya Makongo
PICHA ZAIDI
Wanafunzi wakimsikiliza kwa makini 'The Superwoman'

Nikisisitiza jambo ndani mjadala huo


Vicheko vya hapa na pale ndani ya mjadala


No comments