Header Ads

Kauli Ya Diamond Yamfanya Mrisho Mpotot Asitishe Kutoa Video Yake Ya 'Sizonje'

Kauli ya staa wa muziki Diamond Platnumz ‘Kuna kushoot video na kurekodiwa’ imemfanya msanii wa muziki wa asili Mrisho Mpoto kuitia kapuni kwanza video yake mpya ya wimbo ‘Sizonje’ ili aichunguze kwanza kama inafaa.
Mpoto
Kupitia ukurasa wa instagram, Mpoto ameandika.
Diamondplatnumz post yako ya leo imenifanya nisile Siku nzima. Nikiitafakari na sasa nimeamua kusitisha kutoa video yangu mpya ya #SIZONJE maana sina uhakika kama nime shoot au nimerecord. “Ukimkimbiza sana mjusi anageuka kuwa nyoka
Ijumaa hii Diamond aliachia video mpya ya wimbo ‘Make Me Sing’ akiwa na AKA wa Africa kusini na kutwitter.

No comments