Zari Aaandaa Mpango Kuwasaidia Wanawake wa Dar...Ajipanga Kujenga Kliniki ya Wanawake.

Kupitia ukurasa wa instagram wa Zari ameandika “Wapendwa wangu Sina cha kuwalipa zaidi ya kusema ASANTENI sana kwa 4M followers. ninyi ni ndugu kwangu, mmekua nami bega kwa bega kwenye shida na raha”
“Sasa Mnichiangieni $1 kila mtu tujenge clinic ya wanawake sehemu yoyote dar, Najua tukiipata Baba Magufuli atatupa kiwanja….😁😁 #JustSayingPENDA SANA NYINYI.❤THANK YOU SO MUCH FOR 4M.
LOVE YOU ALL🌹”
Zari ametoa mawazo hayo na kusema kuwa endapo mashabiki hao millioni 4 watafanikiwa kufikisha kiwango flani cha fedha basi Rais JPM hatoshindwa kutoa kiwanja kwaajili ya kujenga kliniki hiyo itakayowasaidia wanawake lakini hajaweka wazi itakuwa inahusika na kutibu magonjwa gani zaidi.

Post a Comment